Orodha ya Mambo ya Kufanya ni nzuri kwa mambo kama kupanga hatua zifuatazo za utafiti au mawazo au maswali ambayo ungependa kujibu kuhusu wahenga maalum.
Jinsi inavyofanya kazi:
Ili kupata kipengele cha Mambo ya Kufanya:
Kwenye tovuti FamilySearch.org, baada ya kuingia, Orodha ya Mambo ya Kufanya iko kwenye kona ya chini kulia ya skrini.
Kuongeza Mambo ya Kufanya:
1. Chagua + Ongeza kitu... katika uga juu ya kisanduku cha Orodha ya Mambo ya Kufanya.
2. Andika katika Mambo yako ya Kufanya.
3. Gusa au bofya alama ya tiki ili kuhifadhi.
Kumbuka: Kikomo cha herufi ni takribani herufi 1000, inategemea na lugha.
Kuhariri au kufuta Mambo ya Kufanya:
1. Tafuta Mambo ya Kufanya ambayo ungependa kuhariri au kufuta.
2. Upande wa kulia wa kipengee cha Mambo ya Kufanya, gusa au bofya nukta 3.
3. Gusa au bofya Haririili kufanya mabadiliko kwenye Mambo ya Kufanya au Futaili kuiondoa kutoka kwenye orodha.
Vitu Vilivyokamilishwa
Mara unapoweka alama ya tiki kipengele cha kufanya, kitaonekana katika orodha ya Vipengele Vilivyokamilika. Vipengele vilivyokamilishwa vinaweza kufutwa kwa kugusa au kubofya ikoni ya kopo la taka.
Viungo katika vipengele vya Mambo ya Kufanya
Unaweza kujumuisha viungo vya kurasa za wavuti au kwa watu katika Mti wa Familia kwenye Mambo ya Kufanya yako. Viungo hivi vinaweza kutenda kama njia ya mkato ili kuruka hadi kwenye eneo la mahali unayotaka kufanyia kazi.
Muhtasari: Maelekezo haya ni kwa ajili ya Orodha ya Mambo ya Kufanya kwenye ukurasa mpya wa nyumbani (hakikisha kitufe karibu na Jaribu vipengele vipya vya ukurasa wa nyumbani kwenye kona ya juu kulia mwa skrini iko upande wa kulia, au kimewashwa). Chaguo la Orodha ya Mambo ya Kufanya halipatikani kwenye aplikesheni ya simu ya mkononi, linapatikana tu kwenye tovuti FamilySearch.org.