Miti ya kundi la familia ni aina ya kundi la familia ambalo huruhusu familia kufanya kazi pamoja katika Mti wa Familia. Katika mti wa kundi la familia, washiriki wa kundi wanaweza kuongeza au kurekebisha taarifa kuhusu watu walio hai ndani ya mti ule ule. Hii hujumisha kuweza kuongeza na kutazama kumbukumbu na vyanzo—kila kitu unachoweza kufanya sasa wa watu waliofariki. Katika mti wa kundi la familia, washiriki wote wa kundi wanaweza kuona na kuhariri watu wale wale, ikijumuisha watu walio hai.
Kwa miti ya kundi la familia, tunatumaini kuwapatia watumiaji wa FamilySearch na manufaa kadhaa muhimu.
Kuunganisha familia yako iliyo hai. Kuza umoja.
Kusanya familia yako katika kundi, na kuona ukoo ule ule. Husisha familia yako katika kushughulikia historia ya familia yao kama timu. Istawishe historia yako na picha, hadithi, na vyanzo.
Shiriki na linda.
Shiriki kumbukumbu na mambo muhimu wakati bado yako akilini, na kulinda faragha ya kila mmoja mtandaoni.
Acha urithi.
Hakikisha kwamba vizazi vya siku za usoni vya familia yako vinaweza kufikia taarifa hii ili kujifunza kuhusu maisha yako.