Je, ni kwa jinsi ninampanga mtu wa kuanzia katika mti wa kundi la familia?

Share

Ikiwa wewe upo kwenye mti wa kundi la familia, ni muhimu kwa mti huu kujua ni mtu yupi anayewawakilisha. Wasifu ambao unakuwakilisha wewe katika mti wa kundi la familia unapaswa kuwa umechaguliwa wakati wewe ulipojiunga au wakati wa kutengenezwa mti wa kundi la familia. Ikiwa hili halikufanywa kwa usahihi, unaweza kubadilisha mtu wa kuanzia.

Hatua (tovuti)

  1. Wakati umeingia kwenye FamilySearch, bofya jina lako hapo pembeni juu kulia.
  2. Bofya Makundi ya Familia.
  3. Bofya kundi la familia.
  4. Katika Mipangilio ya Kundi na Mti, bofya Mtu wa Kuanzia.
  5. Bofya Badilisha.
  6. Tafuta jina lako kwenye orodha, na bofya Chagua.
  7. Hakikisha kwamba mtu huyu ni sahihi, na bofya Ndiyo, Endelea

Hatua (simu ya mkononi)

Kwa sasa, hauwezi kubadilisha mtu wa kuanzia katika app ya Mti wa Familia ya simu ya mkononi. Badala yake tumia tovuti.

Makala zinazohusiana

Je, ni kwa jinsi ninawatagi watu katika miti ya kikundi cha familia?

moduleTitle